Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv umefungwa kwa muda kutokana na kile ambacho kimetajwa kama uwezekano wa kutokea kwa shambulio la angani.
Hatua hii ya Washington inakuja pia baada ya Urusi kuahidi kujibu kufuatia hatua ya Ukraine kupewa idhini ya kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya Moscow kwa mara ya kwanza.
“Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv umepokea taarifa muhimu za uwezekano wa kutokea kwa shambulio la angani Novemba 20,” imesoma taarifa kwenye wavuti wa Marekani.
Kutokana na hilo ubalozi huyo umewaagiza wafanyikazi wake kuchukua tahadhari ya kujikinga kwa sababu za kiusalama.
Urusi ilionya kwamba itajibu kwa nguvu baada ya Ukraine kutekeleza mashambulio ya makombora ya masafa marefu ya Marekani katika ardhi yake.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Kyiv kutumia makombora hayo baada ya karibia kipindi cha miaka mitatu ya mapigano.
Afisa ngazi wa juu wa Ukraine aliiambia AFP kwa shambulio katika mji wa Bryansk nchini Urusi lilitekelezwa kwa kutumia makombora ya ATACMS ya nchini Marekani.