Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Hapi, amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha kulalamika na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kuwasilisha na kueleza ajenda za maendeleo kwa wananchi.
Hapi alitoa kauli hiyo katika mkutano wa wa uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba huku akisisitiza umuhimu wa siasa za hoja zenye tija kwa maendeleo ya taifa, na kusema kuwa malalamiko ya mara kwa mara hayaleti manufaa yoyote kwa wananchi kwani wananchi hawahitaji kusikia porojo wanataka maendeleo
Hapi aliongeza kuwa badala ya kuendelea kulalamika, vyama vya upinzani vinapaswa kuonyesha mfano kwa kueleza mipango na mikakati yao ya kuleta maendeleo kwa jamii.