Kamati ya wataalam wa masuala ya afya inakutana baadae leo kutathmini iwapo mpox bado ishughulikiwe katika kiwango cha dharura ya kimataifa.
Takwimu za Shirika la Afya Duiani WHO zinasema ugonjwa huo umeripotiwa katika takriban mataifa 24 ya kiafrika mwaka huu.
Kwa mujibu wa WHO kumekuwa na matukio zaidi ya visa elfu kumi na tano ya maambukizi ya mpox na wagonjwa 77 wamefariki baada ya kupata maambukizi.
Nchi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa huo ni Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo.
Kwa sasa hali ya kusambaa kwa ugonjwa huo yaonekana imedhibitiwa ingawa viwango vya upimaji pia vimepungua.
Matumaini yapo katika kujaribu kuzuia mpox kwa kutoa chanjo hasa kwa walio katika mazingira hatarishi zaidi.
Hata hivyo chanjo kwa watoto bado haijaifikia Jamhuri ya kidemocrasi ya Congo.