Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza Alhamisi, Novemba 21, kwamba vikosi vyake viliishambulia Ukraine kwa kombora jipya la masafa ya kati, baada ya kushambulia mji wa Dnipro ambapo kombora hilo halikuwa na kichwa cha nyuklia. “Wahandisi wetu wameliita Oreshnik,” Vladimir Putin amesema katika hotuba kwa taifa.
Kulingana na rais wa Urusi, shambulio hili ulimelenga “eneo la kiwanda cha jeshi la Ukraine”.
Katika hotuba yake iliyochukua chini ya dakika 10, rais wa Urusi ameshutumu mashambulio mawili ya hivi majuzi yaliyofanywa na Ukraine katika ardhi ya Urusi kwa kutumia makombora ya Marekani ya ATACMS na ya Uingereza ya Storm Shadow na kuzingatia kwamba mzozo wa Ukraine umechukua “tabia ya kimataifa”, kwa kuwajibisha Watu wa Magharibi ambao waliidhinisha matumizi ya makombora ya Marekani na Ulaya kwenye ardhi ya Urusi.
“Tangu [makombora haya yaliporushwa nchini Urusi], na kama tulivyosisitiza mara kwa mara (hapo awali), mzozo uliochochewa na nchi za Magharibi nchini Ukraine ulichukua sura ya [mgogoro] wa asili ya ulimwengu,” rais wa Urusi amesema. , akibainisha hata hivyo kwamba mashambulio ya makombora ya Magharibi yaliyorushwa na Ukraine kuelekea ardhi ya Urusi yameshindwa.