Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika mpango wao wa kukuza somo la Hisabati kwa shule za Singida akisema kuwa ni mfano bora na ubunifu ambapo Taasisi hiyo inaufanya kukuza elimu hapa nchini.
Ameyasema hayo hapo jana wakati wa Mahafali ya 22 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika katika tawi lao mkoani Singida.
Kwa upande wake Renatus Msagira akimuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Profesa Jehovaness Aikael amesema jukumu walilopewa ni kuishauri Taasisi ya TIA ili itekeleze malengo ya Serikali yaliyoannzisha Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Akiweka wazi kua chuo hiko kinajukumu la kutoa mafunzo yenye ufanisi na ushindani pamoja na kufanya tafiti mbalimbali zenye kunufaisha jamii.
Aidha Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William Amos Pallangyo amesema kuwa mahafali hiyo imehusisha wahitimu 14,77 wa Kampasi ya Singida wakiwemo wanawake 812 huku wanaume wakiwa 665 akisema kuwa ni sawa na asilimia 13 ya wahitimu wote ambao ni elfu kumi na moja mia sita na ishirini (11620) wa Kampasi ya Dar es Salam, Mtwara, Mbeya Mwanza ,Kigoma na Singida.
Taasisi hiyo pia imezindua program ya Masters iliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Singida.