Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya dola, imekamata jumla ya kilogramu 2,207.56 za dawa za kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika Mikoa ya Tanga na Dar es salaam ambapo Watuhumiwa saba wanashikiliwa kuhusiana na dawa hizo.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo November 25,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema
Kati ya dawa zilizokamatwa, skanka ni kilogramu 1,500.6, methamphetamine kilogramu 687.76, heroin kilogramu 19.20, na chupa 10 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl.
Tazama zaidi….