Idadi yatajwa kuongezeka kwa watoto kundikishwa kwenye magenge ya kihalifu nchini Haiti, hii ni kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwalinda watoto (UNICEF) limesema, na kusisitiza hali mbaya ya mzozo wa ulinzi katika kisiwa hicho cha Caribbean kinachokumbwa na ghasia.
Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu, UNICEF ilisema uajiri wa watoto wadogo uliongezeka kwa asilimia 70 mwaka jana.
“Watoto nchini Haiti wamenaswa katika hali mbaya – wameandikishwa katika makundi yenye silaha ambayo yanachochea kukata tamaa kwao, na idadi inaongezeka,” alisema mkurugenzi mtendaji wa UNICEF na mtetezi mkuu wa Kamati ya Kudumu ya Mashirika ya Kimataifa ya Haiti, Catherine Russell. “Mtindo huu usiokubalika lazima ubadilishwe kwa kuhakikisha usalama na ustawi wa watoto vinapewa kipaumbele na wahusika wote.”
Ripoti hiyo inakuja wakati ghasia nchini Haiti hazionyeshi dalili ya kupungua huku umaskini ukiongezeka na machafuko yakiongezeka huku kukiwa na hali ya sintofahamu ya kisiasa. Magenge, ambayo yanadhibiti asilimia 85 ya mji mkuu wa Port-au-Prince, yanalenga kutwaa udhibiti kamili wa jiji hilo.
Wavulana wadogo mara nyingi hutumiwa kama watoa taarifa “kwa sababu hawaonekani na hawaonekani kama tishio”, alisema Geeta Narayan, mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti. Wengine hupewa silaha na kulazimishwa kushiriki katika mashambulizi.
Wasichana, wakati huo huo, wanalazimika kupika, kusafisha na hata kutumiwa kama wanaoitwa “wake” kwa washiriki wa genge.