Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Lushoto Bi. Ikupa Mwasyoge, ameeleza kuwa vituo vya kupiga kura vimeongezeka na kufikia 1,005 Ili kuondokana na changamoto ya umbali mrefu huku akithibitisha kuwa maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika.
Pia, Bi. Ikupa ameeleza kuwa watu wenye mahitaji maalum watapewa kipaumbele ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki. Kuhusu vyama vya siasa, amebainisha kuwa “vyama vinne, yaani CCM, CHADEMA, CUF, na ACT, vimeleta mawakala wao ambao tayari wameapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo”
Katika juhudi za kuwahamasisha wananchi, hususani vijana, Bi. Ikupa amesema wameendesha mabonanza mbalimbali ya michezo Kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi.
Uchaguzi huu ni fursa muhimu kwa wananchi kuchagua viongozi wa mitaa wanaowakilisha maslahi yao.