Tasisi ya Abilisi Foundation imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope FDH kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Uwezeshaji wa wanawake na wasichana Wenye ulemavu katika Uongozi wa kukuza Demokrasia.
Akiwajengea uwezo wa Mafunzo ya siku Moja jijini Dodoma Watendaji wa Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope FDH Mwezeshaji Kutoka Abilisi Foundation Yasin Shehaghilo alisema wamekuwa na Mafunzo Hayo Kwa FDH kwani Taasisi hiyo umepata Ruzuku Kutoka Abilis Fundation Kwaajili ya Mradi ambao wameomba Kwaajili ya kusaidia Jamii Katika Maeneo mbalimbali ya Elimu Ili kuhamasisha wanawake na wasichana Wenye ulemavu washiriki katika chaguzi zijazo ikiwa ni pamoja na kugombea ili wagombee na wapate nafasi ya kuongoza.
Shehaghilo alisema katika mkoa huo wa Dodoma taasisi hiyo ya Abilis foundation kutoka nchini Finland yenye ofisi zake katika Jijiji la Arusha tayari wametoa ruzuku Katika vikundi na Taasisi za Watu Wenye mahitaji maalum zaidi ya kumi.
Shehaghilo alisema mradi huo wa Uwezeshaji wa wanawake na wasichana Wenye ulemavu katika Uongozi Katika kukuza Demokrasia Nchini Tanzania unalenga kufanyika Katika Wilaya Kondoa Katika kata tatu na Dodoma mjini Katika kata Moja kuzitaja kata hizo za Mradi Wilaya ya Kondoa ni Kilimani, Chemchem na kata ya Borisa Kwa upande wa Dodoma ni kata ya Mpunguzi.
Mafunzo haya ambayo yamefanyika hapa Dodoma Katika Ofisi za Taasisi ya FDH zilizopo Ipagala Ilazo West yatawasaidia kwenda Kutoa Elimu Kwa wanawake na wasichana na Watu Wenye ulemavu katika Uongozi na kukuza Demokrasia Hasa Katika kuelekea Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika mwakani Mwaka 2025, Uchaguzi utakao chagua Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani, Wabunge na Rais.
Shehaghilo alisema Elimu hiyo ambayo itatolewa na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope FDH Katika Wilaya ya kondoa na Dodoma mjini hivyo itasaidia Wananchi Kuwa na uelewa wa Nini ambacho wanapaswa kukifanya Katika Jamii Zao na kuweza Kuwa na uelewa mpana Kuhusu mambo ya ulemavu na mahitaji mbalimbali Katika Jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope FDH MAIKO SALALI alisema anashukuru Taasisi ya Abilisi Foundation Kwa kuwapatia Ruzuku Kwa kuona na kuthamini makundi ya Watu Wenye ulemavu kupitia Taasisi ya FDH na kuweza kutoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuweza kuwapatia kipaumbela Kwa kuwapa Mradi ambao utawasaidia Katika Uwezeshaji wa wanawake na wasichana na Wenye ulemavu katika Uongozi kukuza Demokrasia Nchini Tanzania ambapo wataweza.
Aidha Salali aliongeza Kuwa matarajio Yao Katika Mradi Huo ni kuweza kuwafikia wanawake Wenye ulemavu katika Wilaya ya Kondoa na kuweza kuwajengea uwezo Ili waweze kupambana na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.
“Tunataka kuona Jamii ya Watu Wenye ulemavu imeelimika ,Jamii ya Watu Wenye ulemavu imechukua hatua za na kuchangamkia fursa Mbalimbali ambazo zipo Katika Jamii Zao “alisema Salali.
Hivyo kupitia huu Mradi wa Abilisi utawezesha Sasa Watu Wenye ulemavu katika Halmashauri ya Kondoa na Dodoma Kwa ujumla kuweza kupashana habari na kubadilishana mbinu za kuweza kuhakikisha kwamba Kwa Pamoja wanashiriki Katika hutatuzi wa changamoto na hatimaye waweze kupata Viongozi wengi Wenye ulemavu Ili wabebe Ajenda za Watu Wenye ulemavu na kuweza kufikia Malengo ya Pamoja kuhakikisha kundi la mtu mwenye ulemavu linakuwa limepewa nafasi na halimchi mtu kwenye fursa mbalimbali.
Katika hatua Nyingine Salali amehahidi Kufanya kazi Kwa ufanisi na weledi Mkubwa uliotukuka kwani dhamira yao ya pamoja ya Abilisi Foundation na Foundation for Disabilities Hope FDH inaweza kutimia Kwa kuwasaidia Watu Wenye ulemavu waweze kupata haki na kuweza kukua kiustawi.
Alisema kama Shirika wamejipanga kwani wanao watendaji wakutosha ambao watawezesha utekelezaji wa Mradi huu.
Alisema Kuwa muda wa Mradi huu walioupata Kutoka Kwa wadau wa Taasisi ya Abilisi Foundation utatekelezwa ndani ya Mwaka mzima kuanzia November 2024 Hadi November 2025