Idadi ya waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika soko la Kariakoo, imefikia watu 29 baada ya miili tisa kupatikana.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na vyombo vya habari leo, amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati wa shughuli za kuondoa kifusi.
Vilevile Makoba amesema kuwa shughuli za uokozi zimefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.