Iran ilikaribisha usitishaji vita kati ya Israel na Hezbollah ya Lebanon, mshirika mkuu wa wanamgambo wa Tehran huko Mideast.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baghaei alisifu usitishaji huo wa mapigano katika taarifa yake Jumatano asubuhi.
Baghaei alisema kuwa Iran bado inatafuta kusitisha mapigano katika vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Lakini kama Hezbollah, imetupilia mbali madai kwamba usitishaji mapigano pia ufanyike wakati huo huo katika Ukanda wa Gaza.
Pia ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuwahukumu “wahalifu wa utawala unaoukalia kwa mabavu,” akimaanisha Israel.
Mahakama ya ICC imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Israel