Wanaharakati sita wa Cambodia walioshtakiwa kwa uhaini kutokana na maoni yao ya Facebook yanayoikosoa serikali yao wamefukuzwa nchini Thailand ili kujibu mashtaka, kundi linalounga mkono demokrasia lilisema Alhamisi.
Khmer Movement for Democracy, vuguvugu lililoundwa na viongozi wa upinzani walio uhamishoni, lilikosoa uamuzi wa kuwarejesha wanawake hao wanne na wanaume wawili Novemba 24, likisema watakabiliwa na “matendo ya kinyama na ya kudhalilisha” katika mfumo wa magereza uliojaa watu wengi nchini Cambodia.
Thailand na Cambodia zinashutumiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kuwa na makubaliano ya kweli ya kuwarejesha wapinzani wa kisiasa wanaotafutwa na nchi yao.
Wanaharakati hao – Pen Chan Sangkream, Hong An, Mean Chanthon, Yin Chanthou, Soeung Khunthea na Vorn Chanratana – wanahusishwa na chama cha upinzani cha Cambodian National Rescue Party, ambacho kilivunjwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2018 kama sehemu ya kukandamiza upinzani.