Mazungumzo kuhusu kandarasi mpya yanaendelea kati ya wawakilishi wa Lionel Messi na Inter Miami, kwa ujibu wa ripoti mbalimbali.
Klabu hiyo ya MLS inaripotiwa kuwa “inafanya kazi bila kuchoka” kumsaini mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 37 kwa mkataba mpya, huku kukiwa na mipango ya kuhakikisha mustakabali wake katika klabu hiyo hadi 2026.
The Herons, ambao hivi karibuni walimteua mchezaji mwenza wa zamani wa Messi Javier Mascherano kama kocha mkuu, pia alitangaza kwamba mshambuliaji Luis Suárez alitia saini kandarasi mpya ya mwaka mmoja katika uwanja wa Chase Stadium Jumatano.
Mmiliki mwenza wa Inter Miami Jorge Mas pia amesema kuwa “anatarajia” Messi kusalia katika klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika mwaka ujao.