Shinikizo la kijamii la kuanzisha familia limewalazimu Vijana wengi Nchini Vietnam kukodisha Wapenzi wa muda (Fake Boyfriends) ili kuridhisha Wazazi wao na Kulingana na ripoti mwelekeo huu umekuza Biashara mpya ambapo Vijana wanatafuta wenza wa muda kwa matukio maalum kama mikutano ya kifamilia na sherehe za mwaka mpya.
Minh Thu, msichana mwenye umri wa miaka 30 alikodi Mchumba wa muda wakati wa sherehe ya Mwaka Mpya wa Lunar Nchini humo ili kuwaridhisha Wazazi wake waliokuwa wakimtaka awe na mwenza ambapo Mchumba huyo alijitokeza akiwa na ujuzi wa kupika na ustadi wa mazungumzo jambo lililowavutia sana Wazazi wake.
Hali kama hiyo ilimpata pia Msichana Khanh Ngoc ambaye alikodisha kijana wa kuvutia ili kuondoa presha kutoka kwa Familia yake kuhusu ndoa ambapo tukio hilo liliongeza uelewano kati yake na Wazazi wake ingawa ukweli wa mpango huo uliachwa siri.
Biashara ya wapenzi wa muda (fake boyfriemds) imepata umaarufu ikiongozwa na Vijana kama Huy Tuan ambaye anapokea mafunzo ya kuhakikisha anafanikisha matarajio ya Wateja wake hata hivyo licha ya mafanikio yake Wataalamu wanaonya kuhusu athari za kihisia na hatari za kisheria ikiwa mipango hiyo itafichuliwa.
Wachambuzi wanasema kuwa mwenendo huu unaonyesha jinsi Vijana wanavyokabiliana na matarajio ya kijamii na shinikizo la Familia huku wakijaribu kulinda uhuru wao wa kibinafsi Ingawaje baadhi wanaona hatua hii kama suluhisho la muda wakihofia athari za muda mrefu kwa mahusiano ya kifamilia.