Kutokana na hali ya udumavu nchini Wizara saba cana nchini pamoja na taasisi za utafiti zimekutana kwenye kikao kazi cha Wataalam katika kujadili masuala ya huduma za afya na lishe shuleni ambapo wamejikita katika utekelezaji ambao utaleta matokeo katika sekta ya elimu.
Hayo yamejiri mjini Morogoro wakati wa Program ya Taifa ya huduma za Afya na lishe shuleni yenye lengo la kutokomeza hali ya udumavu nchini kwenye jamii kwa ujumla.
Dkt Ntuli Kapologwe Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka wizara ya afya ameeleza uwekezaji kwa watoto waliopo shuleni ni uwekezaji wenye matokeo mazuri hivyo elimu ya afya na lishe ni muhimu katika kujenga taifa la kesho.
Amesema ili Mwanafunzi awe na uwezo wa kufaulu darasani ni lazima awe na afya njema ambayo itamabatana na kupata chakula bora kwa wakati.
Aidha, Alhaj Abdul Maulid Mkurugenzi wa Elimu/Msingi kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia ameeleza Lishe shuleni ni muhimu kwani wanafunzi wataondokana na udumavu huku akitoa wito kwa wazazi kuchangia chakula shuleni kwani ni wajibu wao.
Kwa upande wake Dkt Moke Magoma amesema kufanikiwa kwa huduma za afya na lishe shuleni kutaleta mabadiliko makubwa kwani vijana walio wengi hawana uelewa katika masuala ya afya.
Naye,Dkt Nyamizi Bundala Mkurugenzi msaidizi wa mifugo usalama wa chakula na lishe kutoka wizara ya mifugo na uvuvi amesema kama wizara wanatekeleza mpango wa unywaji wa maziwa shuleni ambapo hadi sasa wamezifikia shule 140 huku matarajio yakiwa ni kufikia shule 5000.
Amesema mfano katika suala la afya na lishe shuleni tunatekeleza mpango wa unywaji maziwa shuleni na tayari ushasambazwa kwa wadau kwa ajili ya kulinda afya za wanafunzi lakini sio maziwa pekee bali watatoa dagaa, mayai na mazao mengine.
Hata hivyo,Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameingia mkataba na wakuu wa mikoa kuhakikisha kila shule inatoa chakula kwa wanafunzi kwa ajili ya kuthamini afya zao.