Katika kuendeleza kutangaza vivutio vya utalii na utunzaji wa mazingira nchini Wilaya ya Kilombero iliyopo Mkoani Morogoro imefanya tamasha maalum linalofahamika kwa jina la Kilombero Festival ambalo limejumuisha taasisi mbalimbali za utalii,Kilimo na utamaduni.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili Dunstan Kyobya amesema hili ni tamasha la kwanza kufanyika katika wilaya huyo huku lengo ni kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo katika eneo hilo sambamba na kuhamasisha wananchi kuhifhi mazingira hasa bonde la Kilombero ambalo linachangaia zaidi ya asilimia 50 kujaza maji bwawa la Mwalimu Nyerere.
Dc Kyobya amesema mipango wa Serikali ya Wilaya hiyo ni kufanya tamasha hilo kuwa endelevu na kufanyika Kila mwaka Ili kuendelea kuunga mkono suala la Utalii na kuhamasisha pia kilimo cha mkakati ikiwemo viungo .
Kwa Upande wake afisa Maliasili na utalii Wilaya Kilombero amesema tamasha hilo linaakisi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan katika kuipaishi nchi kupitia utalii.
Anasema jitihada mbalimbali zinaendelea Ili kulinda vivutio vilivyopo pamoja na uhifadhi wa mazingira ikiwemo kutoa elimu kwa jamii wanaozunguka maeneo ya uhifadhi na kuwa walinzi wa Maliasili hizo.
Aidha anasema pamoja na Mambo mengine wakazi wa eneo hilo wanapata fursa ya Kufahamu historia Yao Kwa kupitia Michezo ya ngoma za asili.
Nao baadhi ya wakazi w. kilombero akiwemo Juma Songozi Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni amesema tamasha hilo linafaida nyingi ikiwemo kunufaika kibiashara kutokana na wageni wengi kutoka nje ya eneo hilo kuhudhuria.
Anasema vilevile wanapata fursa ya kukutana na Watu mbalimbali na kuongeza Mtandao wa biashara na Watu wengine huku wakishauri liwe linafanyika mara mbili Kwa mwaka.