Mbunge wa Same Magharibi, Mhe. David Mathayo,ameanza ziara ya siku sita katika jimbo la Same Magharibi na kuanza kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi wake.
Akianzia kijiji cha Nasuro kata ya Mwembe mhe,Mathayo ametoa mifuko 100 ya saruji ya kujenga nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Nasuro, shilingi 1,760,000 kwa ajili ya madirisha ya nyumba ya mwalimu pamoja na mabati hamsini ya nyumba hiyo.
Pia, Mhe. Mathayo amekabidhi shilingi 2,000,000 kwa ajili ya milango ya nyumba hiyo ya mwalimu, shilingi 350,000 kwa ajili ya kununua kipimo cha Zahanati, shilingi 400,000 kwa ajili ya pumpu ya kumwagilia bustani ya mbogamboga ya kikundi cha vijana.
Akikabidhi msaada huo mhe.Mathayo amesema fedha hizo ni za kwake na ameamua kuwapunguzia wananchi mzigo wa kuchangishwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
“Mimi kama mbunge wenu nimekuja kutekeleza ahadi zangu zote nilizoahidi mara baada ya kuchaguliwa,heshima ya kiongozi ni huduma yake kwa umma tunajua vipato vyetu sio vingi kwa hiyo sisi viongozi kama wabunge tunapojitolea hivi kusaidiana kwenye shughuli za maendeleo maana yake tunapunguza gharama kubwa ambazo pengine wananchi wangechangia”,Alisema Mathayo
Alisema msaada hu oni kuuunga mkono juhudi za serikali chini ya Rais dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wapiga kura wake wa jimbo la Same Magharibi wanaondokana na adha mbalimbali,
“Fedha hizi nazitoa sio za serikali ni za kwangu kama mbunge kwa sababu sitaki wananchi wangu wasumbuliwe na michango ya mara kwa mara”.Alisema Mathayo
Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Mwembe Hamad Msanga amemshukuru Mheshimiwa Mathayo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Nae Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nasuro Upendo Emmanuel amesema msaada huo umekuja kwa wakati kwani utasaiida kupunguza changamoto ya ukosefu wa nyumba za walimu katika kijiji hicho lakini pia itawaondolea usumbufu wazazi wa kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
Wananchi nao wammeshukuru mheshimiwa Mathayo kwa kutekeleza ahadi na kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo kwa kuwajenge miradi mbalimbali lakini pia kuwawezesha wanawake na vijana kujiajiri.