SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema usafiri wa treni ni biashara kubwa, hivyo haliwezi kuruhusu kushindwa kuifanya.
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema hayo jana asubuhi alipozungumza katika kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa na kituo cha televisheni ya Clouds cha Kampuni ya Clouds Media ya Dar es Salaam
“Kwa mara moja inaposimama treni ni watu karibia 5,000 wanasubiria sio wanaondoka kuendesha magari wanasubiri imekuwa ni treni ya wananchi, hii ndiyo kipimo kwamba kwenye hiki kitu hatuwezi kufeli kwa sababu kwamba hatuwezi kuendeleza,” alisema Kadogosa.
Alisema hadi mwishoni mwa Novemba, mwaka huu walikuwa wamesafirisha watu milioni 1.1 na zaidi na kuwa ndani ya muda wa miezi minne walikuwa wamekusanya zaidi ya Sh bilioni 28 kutokana na mapato ya treni za reli ya kisasa (SGR).