Waziri wa fedha na Mipango Zanzibar Saada Mkuya amesema watawafuta wafanyabiashara zanzibar wanaokwepa kutoa risiti za Kieletronic kwa kudai baadhi ya bidha hazitolewi risiti ama kuwaongezea bei wanunuzi wa bidhaa pindi wanapodai risiti
Mkuya amesema kitendo hicho cha kukwepa kutoa risiti kwa kusema baadhi ya bidha hazitolewi risiti au kuzidisha bei ya bidha ni kitendo cha Uhujumu Uchumi na uhalifu na wenye tabia hizo watachukuliwa hatua za kisheria kwa matendo hayo
Ameyasema hayo forodhani Zanzibar alipowatembelea vijana wanaochupia kwenye maji (Wapiga Makachu) na alipofungua wiki mamlaka ya mapato zanzibar zra ya shukrani kwa mlipa kodi huku akibainisha kila mwaka mamlaka anayozismamia ikiwemo zra huongeza pato.