Upelelezi wa kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili wamiliki watatu wa jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es Salaam bado haujakamilika, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Januari 14,2025.
Kesi hiyo iliitishwa leo kwa ajili ya kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakinu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhini ambapo upande wa Jamhuri uliomba ahirisho la kesi hiyo ili ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika.
Kutokana na ombi hilo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 14,2025.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Leondela Mdete (49) Zenabu Islam (61), mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38), mkazi wa llala.
Wafanyabiashara hao wanadaiwa Novemba 16 mwaka huu Mtaa wa Mchikichi na Kongo, jijini Dar es Salaam kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya watu 31 ambao ni Said Juma, Hussein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, na Chatherine Mbilinyi.
Wengine ni Elton Ndyamkama, Mariam Kapekekepe, Elizabeth Kapekele, Hadija Simba, Frank Maziku, Rashid Yusuf, Ally Omary, Ajuae Iyambilo, Mary Lema, Khatolo Juma, Sabas Swai, Pascal Ndungulu, Brighette Mbembele, Ashery Sanga, Venance Aman, Linus Hasara, Issa Bakari, Lulu Sanga, Happnees Malya na Brown Kabovera.