Uingereza siku ya Jumapili ilitangaza msaada wa pauni milioni 50 (dola milioni 63) kusaidia Wasyria walio hatarini baada ya waasi wiki iliyopita kumpindua Rais Bashar al-Assad.
Mamilioni ya Wasyria wanahitaji msaada wa kibinadamu baada ya zaidi ya muongo mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu miundombinu mingi ya nchi hiyo na kusababisha idadi kubwa ya watu kuyahama makazi yao. Baadhi ya wengi waliokimbia nchi wanarejea kutoka majimbo jirani.
Pauni milioni thelathini zitatoa “msaada wa haraka kwa zaidi ya watu milioni moja ikijumuisha chakula, malazi, huduma ya afya ya dharura, na ulinzi kwa walio hatarini zaidi”, Uingereza ilisema katika taarifa.
Pesa hizo, nyingi zinazosambazwa kupitia njia za Umoja wa Mataifa, zitasaidia “mahitaji yanayoibuka ikiwa ni pamoja na ukarabati wa huduma muhimu kama vile maji, hospitali na shule”.
Ili kuwasaidia Wasyria katika nchi jirani, pauni milioni 10 zitakwenda kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Lebanon na pauni milioni 10 zitakwenda Jordan kupitia WFP na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.
Mamilioni ya Wasyria wanahitaji msaada wa kibinadamu baada ya zaidi ya muongo mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu miundombinu mingi ya nchi hiyo na kusababisha idadi kubwa ya watu kuyahama makazi yao. Baadhi ya wengi waliokimbia nchi wanarejea kutoka majimbo jirani.
Serikali ya mpito ya Syria iliapa tarehe 12 Disemba kuanzisha “utawala wa sheria” baada ya miaka mingi ya dhuluma chini ya rais aliyepinduliwa Bashar Al Assad, huku mataifa saba yenye nguvu ya G7 yakishinikiza kuwepo kwa kipindi cha mpito shirikishi.