Nyota wa kimataifa wa Ufaransa na Real Madrid Kylian Mbappe anakimbizana na muda ili kutinga fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya Pachuca, Jumatano.
Mbappe alipata jeraha katika mechi ya timu hiyo. Dhidi ya Atalanta, mnamo Desemba 10, na alipangwa kutokuwepo kwa siku 10.
Kulingana na habari zilizopokelewa kutoka kwa mwanahabari Fabrizio Romano, Mbappe amefanya mazoezi leo kwenye nyasi, na anatumai kuwa atakuwa tayari kwa mechi ya Jumatano.
Real Madrid inawakosa David Alaba, Dani Carvajal, Eder Militao, na Ferland Mendy, huku huduma za Camavinga zikirejeshwa kwenye mechi ya mwisho ya Vallecano.