Askari wawili katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet Nchini Kenya wamekamatwa baada ya kukutwa wakimchinja Ng’ombe aliyeripotiwa kupotea katika kituo cha Polisi cha Kaptagat.
Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi, Askari hao Chrispus Butali na Samwel Mbugua Njuguna walinaswa wakiwa eneo la tukio ambapo Ng’ombe huyo alipokuwa akichinjwa na Mwanamke mmoja, Josphine Kandie ndiye aliyeripoti kupotea kwa Ng’ombe wake kabla ya kupata taarifa kwamba Ng’ombe huyo alikuwa amechinjwa katika kituo hicho cha polisi.
Tukio hilo liliibua hasira kwa Wakazi wa eneo hilo ambao walivamia kituo cha Polisi wakidai Askari hao wahamishwe pamoja na Mkuu wa Kituo (OCS) lakini hata hivyo Juhudi za Polisi kuwatuliza Wananchi hao zilishindikana.