Jaji wa Brazil ameamuru wimbo wa mwimbaji nyota wa pop wa Uingereza Adele,”Million Years Ago,”ufutwe kwenye majukwaa ya muziki duniani kote ikiwa ni pamoja na huduma za utiririshaji kutokana na madai ya wizi
Amri hiyo inatishia kampuni tanzu za Brazil za Sony Music Entertainment na Universal Music, lebo za Adele, kwa kulipa faini ya $8,000 “kwa kila kitendo cha kutotii.”
Kampuni za muziki, hata hivyo, bado zinaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Amri hiyo ilitolewa na hakimu Victor Torres siku ya Ijumaa, katika Mahakama ya 6 ya Biashara ya Rio de Janeiro.
Amri yake ya awali, iliyopatikana Jumatatu na AFP, inaamuru Sony Music Entertainment na Universal Music kuacha “mara moja hasa kimataifa, kutumia, kutengeneza tena, kuhariri, kusambaza au kufanya biashara ya wimbo huo kwa njia yoyote, au kidigitali.
“Ni alama ya muziki wa Brazili, ambayo… mara nyingi imekuwa ikinakiliwa ili kutunga nyimbo za kimataifa zenye mafanikio,” Fredimio Trotta, wakili wa mtunzi wa Brazil Toninho Geraes ambaye alileta malalamiko ya wizi, aliiambia AFP.
Trotta alisema kampuni yake wiki hii itafanya kazi ili kuhakikisha kuwa watangazaji wa redio na televisheni, na huduma za utiririshaji kote ulimwenguni, wanatahadharishwa kuhusu uamuzi huo wa Brazil.