Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kutoa kwa mara ya kwanza tuzo za uhifadhi na utalii katika hafla itakayofanyika Arusha, Desemba 20 kwa lengo la kutambua mchango wa wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi katika kuhifadhi maliasili za nchi.
Mkurugenzi msaidizi wa usimamizi wa rasilimali watu wizara ya Maliasili na Utalii, Shani Kamala na Afisa Utalii wa wizara hiyo, Maria Nyamsekela wamesema hafla hiyo itahuhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo wasanii.
“Tutawatunuku tuzo wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi, Desemba 20, 2025, Arusha ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta hii ya utalii,” alisema Kamala.