Mwanamume mwenye umri wa miaka 60 alikiri hatia Jumatano kwa kosa lake la kuendesha “kituo cha polisi” cha Kichina huko New York kama sehemu ya kampeni ya siri kufuatilia na kuwanyanyasa wapinzani wa Marekani ambapo China imekanusha kuhusika nae.
Hakuna kinachojulikana kama “vituo vya polisi vya siri,” wizara ya mambo ya nje ya China ilisema siku ya Alhamisi, baada ya mkazi wa New York ambaye waendesha mashtaka wanasema waliendesha kituo kama hicho kukiri hatia ya kula njama kama wakala wa kigeni ambaye hajasajiliwa.
Msemaji wa wizara hiyo Lin Jian amesema China ni nchi yenye utawala wa sheria na imekuwa ikifuata kikamilifu sheria za kimataifa na kuheshimu mamlaka ya mahakama ya nchi zote.
Chen Jinping, 60, anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela kwa kula njama kama wakala haramu wa serikali ya China, Idara ya Sheria ilisema katika taarifa yake.
Chen na mwanamume mwingine, “Harry” Lu Jianwang, walikamatwa Aprili mwaka jana na kushtakiwa kwa kuendesha kituo cha polisi cha siri huko Manhattan kwa Wizara ya Usalama wa Umma ya China.
“Ombi la hatia la leo linamfanya (Chen) kuwajibika kwa juhudi zake za kuthubutu za kuendesha kituo cha polisi cha ng’ambo ambacho hakijatangazwa kwa niaba ya jeshi la polisi la taifa la (China) – dharau ya wazi kwa uhuru wa Marekani,” Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Matthew Olsen alisema.
Robert Wells, afisa mkuu wa FBI, alisema kesi ya Chen “ni ukumbusho mkubwa wa juhudi za hila zilizochukuliwa na serikali (ya China) kutishia, kunyanyasa, na kuwatisha wale wanaozungumza dhidi ya Chama chao cha Kikomunisti.”
“Ukiukaji huu wa wazi hautavumiliwa katika ardhi ya Marekani,” Wells alisema.
Lu amekana mashtaka na anasubiri kesi yake.