Mahakama moja nchini China imemhukumu Mwanaume mmoja, Li, kutolazimika kurudisha yuan 300,000 (takriban milioni 600 za Kitanzania) alizopewa na Mpenzi wake wa zamani, Xu, baada ya kugundua kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mpwa wake.
Li na Xu walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2018 lakini mwaka 2020 Li aligundua kuwa Xu alikuwa akifanya usaliti na Mpwa wake jambo lililomshtua na kumfanya Li kutaka kumaliza uhusiano wao, hata hivyo Xu alimtumia barua ya kuomba msamaha akijutia makosa yake na kumwambia kuwa atajirekebisha.
Baada ya Xu kuomba msamaha pia alimtumia Li yuan 300,000 kama ishara ya kujutia na kumaliza maumivu aliyosababisha ambapo Li alikubali msamaha wake na kuendelea na uhusiano huo.
Ingawaje mwaka 2022, Li aligundua kuwa Xu bado alikuwa na uhusiano na mpwa wake, jambo lililomfanya Li kumaliza uhusiano wao kwa mara ya pili. Baada ya kuvunja uhusiano, Xu alidai kurudishiwa fedha alizompa Li, akidai kuwa fedha hizo zilikuwa ni zawadi ya kigezo kwa ndoa ambayo haikutokea.
Li alikataa kurudisha fedha hizo, akisema kuwa Xu alijua alichokuwa akifanya na alikuwa amempa kwa hiari yake ili kumlipa kwa makosa yake. Mahakama ya Shanghai ilichunguza kesi hiyo na kuamua kuwa fedha hizo zilikuwa ni zawadi ya kujitolea kwa Xu ili kurekebisha uhusiano wao na haziwezi kuhesabiwa kama zawadi ya kigezo. Mahakama ilimwandikia Li ushindi na kumruhusu kutolazimika kurudisha fedha hizo.
Kesi hii imezua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii ya China, ambapo baadhi ya watu waliona kuwa uhusiano wao ulikuwa na machafuko, huku wengine wakiona kuwa fedha hizo zilikuwa ni fidia kwa kupoteza upendo na uaminifu.