Kiungo wa kati wa Chelsea Kiernan Dewsbury-Hall anaelekea kuondoka katika klabu hiyo, miezi sita tu baada ya kusajiliwa kutoka Leicester.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipigiwa upatu kuwa mchezaji muhimu chini ya bosi wake wa zamani Enzo Maresca lakini amekuwa akitumika mara chache na sasa Caught Offside anadai kwamba Arsenal inaweza kumpa njia ya kutoka.
Si The Gunners pekee wanaofuatilia hali hiyo, huku Leicester City, Fulham, Rangers, Tottenham Hotspur, Aston Villa, Newcastle United, Brighton & Hove Albion, Brentford, na Manchester United zikiwa zimeorodheshwa.
Kiernan Dewsbury-Hall alianza maisha yake ya soka huko Nottingham na kuhamia Chelsea katika majira ya joto ya 2024.
Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, ameshindwa kufanya vya kutosha kumshawishi meneja Enzo Maresca kumpa nafasi nzuri zaidi kikosini.