Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema iwapo nchi nyingine zitaleta tishio kwa Urusi, anaamini Urusi ina haki ya kutumia silaha za nyuklia dhidi yao.
Katika mkutano wake wa kila mwaka na vyombo vya habari, amesema, “tunazungumza kuhusu vitisho vya kijeshi vinavyoibuka, kama vile kuibuka kwa mifumo ya kupambana na makombora.”
Kauli hii imekuja mwezi mmoja tangu Kremlin kuidhinisha mabadiliko ya kanuni mpya ambazo nchi hiyo itazizingatia juu ya utumiaji wa silaha zake.
Kanuni mpya zinasema shambulio kutoka kwa taifa lisilo la nyuklia, ikiwa litafanyika chini ya usaidizi wa nchi yenye nguvu za nyuklia, litachukuliwa kama shambulio la pamoja dhidi ya Urusi.