Mahakama ya juu nchini Ghana imetupilia mbali kesi mbili tofauti zilizokuwa zimewasilishwa kama rufaa kupinga mojawapo ya sheria kandamizi zaidi dhidi ya watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Hatua hiyo inatoa fursa kwa rais kusaini mswada na kuwa sheria.
Bunge la nchi hiyo ya Afrika magharibi lilipitisha mswada dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, mwezi Februari.
Sheria hiyo iongeza msako dhidi ya watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja na wanaharakati wanaotetea uhusiano huo.
Hata hivyo, rais Nana Akufo Addo alichelewa kusaini mswada na kuwa sheria baada ya rufaa kuwasilishwa katika mahakama ya juu.
Jqji Avril Lovelance-Johnson, amesoma uamuzi wa jopo la majaji saba, kwamba rufaa iliyowasilishwa haina msingi.
Katika sheria ya sasa, uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ni haramu na una adhabu ya hadi miaka mitatu gerezani. Endapo itasainiwa, sheria ya sasa inapendekeza kifungo cha hadi miaka 5 gerezani.