Gabon imeingia rasmi Jamhuri ya Tano tangu leo Alhamisiasubuhi. Nakala ya Katiba mpya, iliyopitishwa na kura ya maoni mnamo mwezi Novemba, imeidhinishwa mnamo Desemba 19, 2024 na rais wa mpito, wakati wa sherehe iliyoandaliwa kwenye Uwanja wa Ukombozi huko Libreville, mbele ya mnara uliozinduliwa mnamo Agosti 30 kwa heshima ya askari waliompindua Ali Bongo mwaka mmoja kabla.
Katiba mpya ya Gabon itatumika kwa uhakika baada ya uchaguzi, ambao tarehe yake bado haijajulikana lakini ambao utafanyika kabla ya mwezi Agosti 2025.
Katika hotuba yake mnamo Desemba 19, 2024 mjini Libreville, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema amekaribisha ahadi iliyotekelezwa na maendeleo ya mchakato wa kura ya maoni. Amebaini kwamba jamhuri mpya lazima iwe “kinga” cha utawala uliopita: “Ukomavu wa watendaji tofauti, umoja wa kitaifa, uvumilivu, heshima kwa wengine na uwazi ulioenea katika mchakato huu unathibitisha leo kwamba Gabon imepiga hatua kubwa yenye ubora kuelekea enzi mpya. Sheria hii ya msingi inaitwa kuwa kielelezo cha historia yetu na jukwaa la matumaini yetu