Jitihada Za Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa na kutolewa kwa nadharia na Vitendo zaidi ili kuwarahisishia Wahitimu kuweza kujiajiri pindi wakimaliza masomo yao.
Zaidi ya Wanafunzi 200 wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kutokea Ndaki ya usanifu Majengo na Teknolojia ya Majenzi (coACT) wamefanya mafunzo ya Usanifu Majengo kwa Vitendo Mkoani Iringa na wameeleza umuhimu wa mafunzo hayo namna yatakavyokwenda kuleta tija mara baada ya kumaliza masomo yao.
Nao Wakufunzi ambao wameambatana katika Safari hiyo na Wanafunzi hao wamesema kuwa wanaamini kwenye ufundishaji wa Vitendo kwani unamjengea uwezo Mwanafunzi kuweza kujijenga zaidi katika soko la ajira kulingana na fursa zilizopo.
” tunazipongeza juhudi za serikali kwa kutuwekea mazingira rafiki ya sisi wanafunzi kujifunza kuanzia suala la mikopo ”