Mamlaka ya Mji Mkongwe zanzibar imesimamisha shughuli za kuchupia kwenye maji forodhani maarufu upigaji wa makachu kwa kile kinachodaiwa kua ni ukiukwaji wa taratibu zilizoekwa baada ya raiya wa kigeni kupiga makachu na nguo zilizokiuka maadili ya Mzanzibar
Ayo tv imezunguza kwa njia ya simu na mmoja wa wapiga makachu ambao amemulezea mwandishi wa Ayo tv visiwani humo kua chanzo cha kusimamishwa kwa shughuli hizo ni raiya wa kigeni wa marekani kupiga kachu huku akizalia nguo zisizostaha.
Mamlaka inaendelea na uchunguzi wa jambo hilo na. wahusika watakaobainika kufanya vitendo hivyo watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria. Mamlaka kwa kushirikiana na wadau, wakaazi na watumiaji wa Mji Mkongwe, inaziomba Taasisi za Umma na Binafsi pamoja na
wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo kama hivyo ili kuchukuliwa hatua. Kwa
pamoja, tunaweza kulinda na kuendelcza Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni urithi wetu wa kihistoria na kitamaduni.
” Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe inatoa arifa cufuatia matukio ya ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo
yaliyojitokeza kwa vijana wa makachu katika eneo Ia Bustani ya Forodhani, matukio ayo yameleta athari mbaya kwa jamii na miundombinu ya Serikali, Matukio ayo yanajumuisha pigaji makachu kwa kutumia wa mavazi yanayokwenda kinyume na utamaduni, uharibifu mkubwa
wa mifereji na miundombinu mengine pamoja na matumizi ya debe za taka kwa michezo ya vichekesho (Comedy) “