Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, limekamata madini ya dhahabu bandia gramu 250.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema hayo leo, akisema ni baada ya msako ambao umefanywa kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 22, 2024.
Amesema katika msako huo, wamekamata jumla ya watu 81 na vingine ni bangi gramu 9,000, mirungi bunda tisa, gongo lita 113, sola panel saba, betri nne za sola, pikipiki 11, kadi tatu za pikipiki, antena nne za ving’amuzi.
Vingine ni redio mbili, baiskeli mbili, mashine moja ya bonanza, kamera moja na mitambo minne ya kutengeneza gongo.