Mamia ya waandamanaji waliingia barabarani katika maeneo ya Wakristo huko Damascus mapema Jumanne kupinga kuchomwa kwa mti wa Krismasi karibu na Hama katikati mwa Syria, waandishi wa habari walisema.
Maandamano hayo yalizuka baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha wapiganaji waliojifunika kofia wakichoma moto mti wa Krismasi katika mji wenye Wakristo wengi wa Suqaylabiyah, karibu na Hama
“Tunadai haki za Wakristo,” waandamanaji waliimba walipokuwa wakipita katika mji mkuu wa Syria kuelekea makao makuu ya Patriarchate ya Orthodox katika kitongoji cha Bab Sharqi.
Maandamano hayo yanakuja ikiwa ni zaidi ya wiki mbili baada ya muungano wenye silaha unaoongozwa na Waislam kupindua serikali ya Bashar al-Assad, ambaye alijifanya mlinzi wa walio wachache katika nchi hiyo yenye Wasunni wengi.
Mwandamanaji aliyejitaja kwa jina la Georges alisema alikuwa akipinga “ukosefu wa haki dhidi ya Wakristo”.
“Ikiwa haturuhusiwi kuishi imani yetu ya Kikristo katika nchi yetu, kama tulivyokuwa zamani, basi hatuko hapa tena,” alisema