Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amekabidhi zawadi za Siku Kuu ya Krismas kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum katika vituo vya malezi vya Tawfia kilichopo Mhandu Nyamagana na TCRC Nyasaka llemela.
Akizungumza katika nyakati tofauti mara baada ya kukabidhi
zawadi hizo Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Rais kwa kuamua kusherehekea Siku Kuu pamoja na watoto kwa kuwa kumbuka kwa zawadi ili watoto hao wale na kunywa kwa kufurahia pamoja.