Maafisa wa Taliban nchini Afghanistan waliripoti Jumatano kwamba takriban watu 46 waliuawa katika eneo la mpaka wa mashariki kwa sababu ya mlipuko wa angani wa usiku ambao inadaiwa kutekelezwa na Pakistan.
Zabihullah Mujahid, msemaji wa serikali ya Taliban, alisema kuwa shambulio la Jumanne jioni lililenga maeneo manne huko Barmal, wilaya ya mbali ya milima katika mkoa wa mpaka wa Afghanistan wa Paktika.
“Idadi ya jumla ya waliofariki ni 46, wengi wao wakiwa watoto na wanawake,” Mujahid aliliambia shirika la habari la Agence France-Presse, akiongeza kuwa raia sita zaidi walijeruhiwa. Ukweli wa madai yake kuhusu wahasiriwa haukuweza kuthibitishwa kutoka kwa vyanzo huru.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Taliban ilitangaza Jumatano kwamba imemwita kaimu balozi wa Pakistani mjini Kabul kutoa “maelezo makali ya kupinga mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Pakistani” huko Barmal. Taarifa hiyo imelaani shambulio hilo na kuonya kwamba “vitendo kama hivyo vinachukuliwa kuwa vya kutowajibika sana na bila shaka vitaleta athari.” Haikufafanua