Jeshi la Ukraine lilisema Alhamisi kwamba liliangusha ndege 20 kati ya 31 ambazo vikosi vya Urusi vilirusha katika mashambulizi ya usiku.
Mapigano hayo yalifanyika katika maeneo ya Chernihiv, Dnipropetrovsk, Kharkiv na Kyiv, jeshi la anga la Ukraine lilisema.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema Alhamisi iliharibu ndege tano zisizo na rubani za Ukraine katika maeneo ya Volgograd, Voronezh na Belgorod.
Gavana wa Belgorod Vyacheslav Gladkov alisema kwenye Telegram shambulio la ndege isiyo na rubani iliharibu majengo kadhaa ya ghorofa na nyumba, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Duru ya hivi punde ya mashambulio ya angani kati ya pande hizo mbili ilifuatia siku yenye nguvu zaidi kuliko kawaida ya mashambulio ya ndege zisizo na rubani na makombora.
Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumatano alilaani shambulizi kubwa la Urusi ambalo jeshi la Ukraine lilisema ni pamoja na ndege zisizo na rubani 106 na makombora 78.