Ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) Jumatatu wiki hii imesema maambukizi milioni 8.4 ya malaria yameripotiwa nchini Ethiopia tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na ugonjwa huo unaendelea kuhatarisha afya ya umma nchini humo ambapo kwa wastani maambukizi laki 3 ya ugonjwa huo yanaripotiwa kila wiki, karibu kila eneo la nchi hiyo limeripoti maambukizi ya ugonjwa huo.
Malaria ni ugonjwa unaoenea zaidi katika maeneo yaliyo chini ya mwinuko wa mita 2,000 nchini Ethiopia, yakijumuisha robo tatu ya ardhi ya nchi hiyo, na takriban asilimia 69 ya watu wa nchi hiyo wanaoishi katika maeneo hayo wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa.