Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis Jumatano katika hotuba yake ya kawaida wakati wa Krismasi amewasihi “watu wa mataifa yote” kuwa na ujasiri kwenye mwaka huu Mtakatifu, kwa kuzima milio ya silaha na kumaliza migawanyiko inayoikumba dunia, Mashariki ya Kati, Ukraine, Afrika na Asia.
Hotuba hiyo maalum ya Krismasi maarufu kama ‘Urbi et Orbi’ kwa kitaliano au ‘Kwa mji na Dunia’ huangazia baadhi ya masaibu yanayoikumba dunia. Krismasi ya mwaka huu imeendana na mwanzo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa 2015 ambayo amesema yatakuwa ya amani, wakati akiomba maridhiano hata na adui zetu.
“Naomba kila mmoja na watu wa mataifa kuwa mahujaji wa amani, ili kunyamazisha milio ya silaha na kumaliza migawanyiko,” Papa Francis alisema kwenye bustani ya St Peter’s Basilica, mbele ya umati mkubwa watu. Aliomba silaha zikomeshwe kwenye vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, huku pia akisisitiza kuachiliwa kwa mateka wa Israel waliyotekwa na Hamas Oktoba 7, mwaka jana.