Jeshi la anga la Ukraine limeshambulia kituo cha viwanda cha kijeshi katika eneo la Rostov nchini Urusi katika siku chache zilizopita.
Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Ukraine, ambalo halikutoa tarehe ya shambulio hilo wala kufichua uharibifu uliotokea.
Kituo hicho, katika mji wa Kamensk-Shakhtinsky, kinatumika kuzalisha mafuta imara kwa makombora ya balistiki, jeshi la Ukraine lilisema.
Urusi kwa upande mwingine imekuwa ikilenga tu vifaa vya kijeshi na miundombinu, aliongeza vya Ukraine na “sio katika sheria zetu kugonga maeneo ya raia”.
Vikosi vya Urusi vimekuwa vikishutumiwa sana na mara kwa mara kwa kuwalipua raia tangu kuanza uvamizi wa Ukraine karibu miaka mitatu iliyopita, huku majengo ya makazi yakipigwa mara kwa mara na makombora na ndege zisizo na rubani.