Wakati wa sherehe za Krismasi, tukio la kipekee lilitokea huko Fort Collins, Colorado ambapo mwizi aliiba sanamu ya Mtoto Yesu kutoka eneo la Old Town Square na baadae kuirudisha akiambatanisha na ujumbe uliosomeka “haitatokea tena” katika kituo cha zima moto.
Kulingana na gazeti la New York Post, sanamu hiyo ilipotea tangu tarehe 17 Desemba, na kuacha eneo linaloashiria kuzaliwa kwa Yesu halijakamilika.
Hata hivyo, sanamu hiyo ilirejeshwa kwa wakati kwa ajili ya Krismasi, na kuleta hali ya utulivu kwa jamii.
Hapo awali, Idara ya Polisi ya Fort Collins ilitoa picha ya mshukiwa, anayedaiwa kunaswa akiiba sanamu ya Baby Jesus kutoka kwenye mapambo ya kitamaduni ya sikukuu Old Town Square.