Ufaransa imeendelea kushikilia makali yake tangu 2023 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 15 kupata idhini ya wazazi kujiandikisha kwenye mitandao ya kijamii, ambayo inahitajika kutekeleza mfumo wa kuthibitisha ikiwa idhini hiyo imepatikana.
Kulingana na data kutoka kwenye Chama cha E-Enfance cha Kulinda Watoto Mtandaoni, 82% ya watoto wanakabiliwa na maudhui hatari mtandaoni, ikiwa ni pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya, silaha,picha na video zisizofaa.
Zaidi ya hayo, matumizi ya mitandao ya kijamii yamesababisha kuongezeka kwa matukio ya kutengwa na unyanyasaji wa matusi shuleni.
Ripoti ya 2023 e-Enfance inasema kuwa 67% ya watoto wenye umri wa miaka 8-10 na 86% ya wale wenye umri wa miaka 8-18 wanatumia mitandao ya kijamii nchini Ufaransa.
Familia moja kati ya nne nchini Ufaransa pia inakumbana na unyanyasaji wa mtandaoni.
Miongoni mwa watoto wanaofanyiwa unyanyasaji mtandaoni, 51% wanakabiliwa na changamoto katika elimu yao huku 52% wakipata matatizo ya usingizi na kukosa hamu ya kula.
Kadiri watoto wanavyoweza kutumia intaneti na hatari zake kuongezeka kwa kasi, serikali inachukua hatua kulinda afya na haki za watoto.