Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Dkt.Scholastika Kevela amegiza viongozi wa Jumuiya hiyo kufanya kazi ili kuwapelekea maendeleo wanawake na kuzifikia ndoto zao.
Dkt.Scholastika ametoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano wa baraza kuu la UWT mkoa wa Njombe uliofanyika kwenye ukumbi ofisi za Chama hicho mkoa wa Njombe zilizopo mji Mwema katika halmashauri ya mji wa Njombe.
“Viongozi tuwajibike kwa nafasi zetu na tukawatendee haki wanawake waliotupa dhamana ili kazi pia ya kuomba kura kwa ajili ya Rais ikawe nyepesi kwetu”amesema Scholastika
Dkt.Scholastika amesema uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan miradi mingi ya maendeleo inaendeleo kutekelezwa huku utawala bora ukiendelea kuzingatiwa jambo ambalo linapaswa kuigwa na viongozi wengine.
Aidha amesema mkoa wa Njombe bado umeendelea kuwa tishio kwenye matukio ya ukatili jambo ambalo linapaswa kuunganishwa nguvu za pamoja katika jamii ili kukabilia na vitendo hivyo.