Hatimaye Chuo Kikuu Mzumbe Kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kimetolea ufafanuzi juu ya barua inayosambaa mitandaoni ya kijamii ikieleza kuwa chuo hicho kimetangaza wanafunzi ambao hawajakamilisha usajili wa wanufaika wa bodi ya mikopo wameongezewa muda wa usajili hadi Januari 10 mwaka huu 2025 huku wale wanaojilipia ada muda wao wa usajili ulishamalizika tangu Disemba 30, mwaka jana 2024 na kwa Sasa wanatakiwa kuandika barua za kuahirisha mwaka wa masomo.
Makamu mkuu wa chuo Kikuu Mzumbe Pro. William Mwegoha amesema taarifa hiyo si msimamo wa chuo na kwa sasa wanaendelea na taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu Prof. Eliza Mwakasangula ambaye ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mzumbe anayeshugulikia taaluma ,utafiti na ushauri kitaalam ambaye ndiye aliyeiandika barua hiyo kwamba tayari uchunguzi unafanyika kwa mtumishi huyo Ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Prof. Mwegoha amesema kwa Sasa Chuo kinaomba radhi kwa barua hiyo ambayo imeleta taharuki katika jamii na sasa udahili unaendelea kaka kama kawaida Hadi January 10 mwaka huu.