Watu wasiojulikana wamechoma ofisi ya mtendaji wa kata ya Silambo wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora na kusababisha uharibifu wa jengo la ofisi na kuteketea kwa nyaraka zote za serikali zilizokuwa zinahifadhiwa kwenye ofisi hiyo.
Ayo TV imefika katika kata ya Silambo eneo la tukio na kushuhudia uharibifu huo huku Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Mongella akiwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuharibu mali za Umma.
“Kama Kuna baadhi ya watu hawamkubari Mtendaji na kufanya uharibifu wa namna hii basi wamekosea sana jambo hili haliko Sawa,hii ofisi haikuwa Mali ya serikali msamalia mwema tu alitusaidia ikapatikana lakini leo hii kati yenu hapo mmeichoma,Sasa sisi tu taangalia namna ya Kurejesha hii nyumba ya watu,Ila Kwa yoyote atakayebainika kuhusika na tukio hili serikali haitomuacha na hatua Kari za kisheria zitachukuliwa juu yake.
Akizungumzia tukio Hilo diwani wa kata ya hiyo Mashaka Mpuya amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Kuna baadhi ya wananchi hawamkubari na hawamtaki Mtendaji wa kata hiyo huku mkuu wa Polisi wilaya ya kaliua mrakibu mwandamizi wa Polisi Mahemba Kavalambi akionesha mashaka yake juu ya tukio hilo na kuahidi kuwasaka wote waliohusika na tukio hilo.