Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita kimesema hakilidhishwi na kasi ya Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami wa 17km Barabara zinazojengwa katika Manispaa ya Geita zenye thamani ya shilingi Bilioni 22.5 Fedha kutoka Benki kuu ya Dunia.
Kauri hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita, Barnabas Mapande mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo unaojengwa na kampuni ya wachina Sechan Road and Bridge Ltd ambapo mradi huo upo aslimia 26 na hauridhishi kutokana na Matakwa ya Mkataba.
“Niseme tuu kwamba mradi huu huu mradi unakosa neno la kuzungumza kwasababu ni mradi ambao unaleta Masikitiko makubwa sana ukiusema sana unaweza ukajikuta umetumia neno ambalo wengine wakaona kama vile unatukana lakini ukweli ni kwamba mradi huu unatia kichefu chefu , ” Mwenyekiti CCM wilaya ya Geita, Barnabas Mapande .
” Taarifa inajieleza kwa kulalamika taarifa inajieleza kwa kumlalamikia mkandarasi kwa kutokutimiza matakwa ya mkataba kwahiyo katika taarifa hii tunaiona wazi kabisa inamlalamikia mkandarasi Mhandisi mshauri na tumesikia kiongozi wetu mkurugenzi kazungumza hapa hoja ni mkandarasi kutokutimiza matakwa ya mkataba na mradi , ” Mwenyekiti CCM wilaya ya Geita, Barnabas Mapande.