Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alisema Jumapili Kyiv iko tayari kuwakabidhi wanajeshi wa Korea Kaskazini waliotekwa kwa kiongozi wao Kim Jong Un ikiwa ataweza kuwezesha kubadilishana kwao na Waukreni waliotekwa nchini Urusi.
“Mbali na wanajeshi wa kwanza waliokamatwa kutoka Korea Kaskazini, bila shaka kutakuwa na zaidi. Ni suala la muda tu kabla ya wanajeshi wetu kuweza kuwakamata wengine,” Zelenskiy alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Akiandika kwenye X, Zelenskyy alisema Ukraine ilikuwa tayari kuwakabidhi wanajeshi hao kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un “kama ataweza kuandaa mabadilishano yao kwa ajili ya wapiganaji wetu wanaozuiliwa nchini Urusi”.
Kiongozi wa Ukrain alisema “bila shaka kutakuwa na askari zaidi” wa Korea Kaskazini waliokamatwa vitani. “Ni suala la muda kabla ya askari wetu kuweza kukamata wengine,” alisema.
Ukraine ilisema siku ya Jumamosi wanajeshi hao wawili walijeruhiwa wakipigana na wanajeshi wake katika eneo la Kursk nchini Urusi.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Kyiv kutangaza kuwakamata wanajeshi wa Korea Kaskazini wakiwa hai tangu waingie kwenye vita vilivyodumu kwa takriban miaka mitatu msimu wa vuli uliopita.