Mwanamuziki mashuhuri na mrembo Queen Bey kupitia Taasisi Yake, Iitwayo “BeyGood”, Imeripotiwa Kuchangia Kiasi Cha $2.5m (Tsh Bilioni 6.3/=) Ili kusaidia Walioathirika na moto mkubwa unaoendelea huko Los Angeles.
BeyGood, Imelenga kuwapa wahanga misaada ya dharura, kama vile chakula, malazi, na huduma za afya ya akili, huku pia ikisaidia miradi ya ujenzi na vitu vingine vingi .
Hatua hii ni mfano wa jinsi mastaa na mashirika yao wanavyoweza kutumia ushawishi wao kusaidia watu walioko kwenye hali ngumu.
Beyoncé amekuwa akisisitiza umuhimu wa kusaidia jamii zilizo na uhitaji mkubwa kupitia Mashirika na kampeni mbalimbali, na mchango huu unadhihirisha dhamira yake ya kusaidia wale walioko katika wakati mgumu.