Uteuzi wa tuzo za Oscar umecheleweshwa kwa wiki moja kutoka tarehe yao ya awali baada ya milipuko inayoendelea huko California na sasa unatarajiwa kutangazwa Januari 23.
Huku moto ukiendelea kushuhudiwa katika eneo la Los Angeles, chuo cha filamu kiliongeza muda wa upigaji kura kwa wanachama wake hadi Ijumaa awali, uteuzi ulipaswa kutangazwa asubuhi
Shirika ambalo huandaa Tuzo za Oscar pia limefanya uamuzi wa kughairi mlo wa mchana wa wateule wake wa kila mwaka, tukio lisiloonyeshwa na televisheni linalojulikana kama“class photos” ambazo hutoka kila mwaka.
Tuzo za Kisayansi na Kiufundi, zilizowekwa hapo awali Februari 18, zitaratibiwa tena baadaye.
Tuzo za 97 za Oscar bado zitafanyika Machi 2, kwenye Ukumbi wa michezo wa Dolby, na matangazo ya moja kwa moja ya televisheni kwenye ABC.